1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken kuhudhuria mkutano kuhusu Haiti

11 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa kukutana na viongozi wa eneo la Karibiani nchini Jamaika kama sehemu ya jitihada za dharura za kuutatua mzozo unaotokota nchini Haiti.

 Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alitazamiwa kuhudhuria mkutano kuhusu Haiti uliofanyika nchini Jamaika.Picha: THOMAS KIENZLE/AFP/Getty Images

Mkutano huo unafanyika wakati shinikizo la kumtaka Waziri Mkuu Ariel Henry ajiuzulu au akubali kuunda baraza la mpito.

Henry, ambaye amezuiwa kurejea nchini mwake baada ya kuongezeka kwa machafuko, alitarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa faragha siku ya Jumatatu (Machi 11).

Soma zaidi: CARICOM yawaalika wanadiplomasia wa mataifa makubwa kuijadili Haiti

Mkutano huo uliandaliwa na wanachama wa Jumuiya ya Kibiashara ya Karibiani (CARICOM), ambayo kwa miezi kadhaa imekuwa ikishinikiza kuundwa kwa serikali ya mpito nchini Haiti, huku waandamanaji wakimtaka Henry ajiuzulu.

Henry aliwasili nchini Puerto Rico wiki iliyopita baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia Jamhuri ya Domikani, taifa jirani la Haiti.

Tayari balozi za kigeni zimewahamisha wafanyakazi wake kutoka mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, kufuatia machafuko ya magenge ya wahalifu yanayosambaa katika mji huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW