1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken kujadili suala la Gaza mjini Istanbul

6 Januari 2024

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken kufanya mazungumzo na rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Instabul Jumamosi.

Bliken akutana na waziri wa Uturuki wa mambo ya nje Hakan Fidan
Bliken akutana na waziri wa Uturuki wa mambo ya nje Hakan Fidan Picha: Evelyn Hockstein/AP/picture alliance

Ajenda kubwa ya mazungumzo itakuwa vita kwenye Ukanda wa Gaza katikati ya kiwingu cha mashaka kuwa mzozo huo unaweza kutanuka na kuwa wa kanda nzima.

Blinken aliwasili Uturuki usiku wa kuamkia leo na anatazamiwa kufanya ziara nyingine eneo la Mashariki ya Kati kwa kuzitembelea Israel, mataifa matano ya kiarabu na kufanya mazungumzo na viongozi wa Palestina huko Ukingo wa Magharibi.

Kabla ya kuelekea kwenda kanda hiyo amepangiwa kwanza kwenda nchini Ugiriki kwa malengo ya kutuliza wasiwasi wa viongozi wa taifa hilo juu ya uwezekano wa Marekani kuiuzia ndege za kivita Uturuki ambayo ni hasimu wa serikali mjini Athens.