1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken kuwasili tena Israel kwa mazungumzo kuhusu Gaza

18 Agosti 2024

Waziri wa Mambo ya Mje wa Marekani, Antony Blinken, anatarajiwa kuwasili Israel hii leo kwa mazungumzo ya kushinikiza kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano huko Gaza.

 Blinken
Waziri wa Mambo ya Mje wa Marekani, Antony Blinken, anatarajiwa kuwasili Israel kwa duru nyingine ya mazungumzo ya kusitisha maoigano GazaPicha: TED ALJIBE/AFP

Waziri wa Mambo ya Mje wa Marekani, Antony Blinken, anatarajiwa kuwasili Israel hii leo kwa mazungumzo ya kushinikiza kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano huko Gaza.

Hii ni safari ya kumi kwa mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani katika eneo hilo tangu kuanza kwa vita hivyo vilivyoanza Oktoba mwaka uliopita na mara hii anarudi tena siku chache baada ya Marekani kuyaweka hadharani mapendekezo ambayo Misri na Qatar zinaamini yatavimaliza vita hivyo.

Soma zaidi. Duru mpya ya mazungumzo kuhusu mzozo wa Gaza

Mawaziri wa mambo ya nje katika mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia katika taarifa yao pamoja wameunga mkono mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano na kuzitaka pande zote kutoweka ugumu katika juhudi hizo.

Hata hivyo, mazungumzo yanafanyika katika ya kiwingu cha kutanuka kwa mzozo wa kikandaambapo Iran inatishia kulipiza kisasi kwa Israel baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, mjini Tehran mnamo Julai 31.