1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken: Mazungumzo yaweza kuwa fursa ya mwisho kwa Gaza

19 Agosti 2024

Antony Blinken amesema siku ya Jumatatu kwamba mazungumzo yanayotarajiwa kuanza wiki hii nchini Misri, yanaweza kuwa "fursa ya mwisho" ya kufikiwa makubaliano ya mzozo wa Gaza.

Israel | Antony Blinken na Isaac Herzog
Blinken ambaye yuko ziarani mjini Tel-Aviv, ikiwa ni ziara yake ya tisa tangu shambulizi la Oktoba 7, amekutana Jumatatu asubuhi na Rais wa Israel Isaac Herzog kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.Picha: Kevin Mohatt/AFP/Getty Images

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema hivi Jumatatu kwamba mazungumzo yanayotarajiwa kuanza wiki hii nchini Misri, yanaweza kuwa "fursa ya mwisho" ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.

Blinken ambaye yuko ziarani mjini Tel-Aviv, ikiwa ni ziara yake ya tisa tangu shambulizi la Oktoba 7, amekutana Jumatatu asubuhi na Rais wa Israel Isaac Herzog kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Marekani, Misri na Qatar wamekuwa wapatanishi katika mfululizo wa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Israel na kundi la Hamas.

Duru za hivi punde za mazungumzo ya siku mbili nchini Qatar zilimalizika bila mafanikio makubwa siku ya Ijumaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW