Blinken: Uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa Senegal
14 Februari 2024Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Matthew Miller, ameweka wazi kuwa wangependa kuona uchaguzi unafanyika kama ulivyopangwa.
Miller pia alisema kuwa Marekani inawasiwasi mkubwa kuhusu hali katika taifa hilo la Afrika Magharibi, ambapo mamlaka Jumanne(13.02.2024) ilizuia mtandao wa simu na kupiga marufuku maandamano.
Kama uchaguzi usipofanyika Februari 25, basi ufanyike haraka
Miller ameongeza kwa kusema Blinken anahimiza uchaguzi ufanyike kwa wakati na ikiwa hautafanyika Februari 25, ungepaswa kufanyika haraka iwezekanavyo baada ya hapo.
Rais Sall amesogeza mbele uchaguzi wa Februari 25, na kusababisha mzozo wa kisiasa nchini Senegal, ambalo kijadi ni thabiti na kutolewa mfano na Blinken kama demokrasia bora kwa Afrika katika ziara yake ya 2021.
Umoja wa Mataifa wataka haki ya kuandamana iheshimiwe
Katika hatua inayofanana na hiyo, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema haki ya Wasenegal kuandamana kwa amani lazima iheshimiwe.
Kauli hiyo ni baada ya mamlaka ya taifa hilo la Afrika kupiga marufuku maandamano kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais. Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema wana wasiwasi sana kuhusu maendeleo ya kwa hali ya amani nchini Senegal.
Soma zaidi: Wabunge wakamatwa wakipinga kuahirishwa uchaguzi Senegal
Aidha amesema ni muhimu sana kwamba Wasenegal wote wawe na haki yao ya kuandamana, kuheshimiwa kwa amani, akitaka hali hiyo "isuluhishwe kupitia njia zilizowekwa za kikatiba ya taifa hilo.
Chanzo: RTR