Blinken ziarani Afrika kupunguza ushawishi wa Urusi
24 Januari 2024Matangazo
Waziri Blinken anayeitembelea Nigeria, katika ziara yake ya barani Afrika, amesema Marekani ipo tayari kuendelea kuisaidia Nigeria na washirika wengine katika juhudi za kuleta utulivu kwenye eneo la Sahel, ambalo limegeuzwa kuwa uwanja hatari wa kigaidi, baada ya mapinduzi kadhaa ya kijeshi kufanyika hivi karibuni.
Blinken amesema mjini Abuja kwamba maendeleo yatapatikana kwa kurejesha utawala wa kikatiba, kwa ushirikiano wa nchi za ukanda wa Sahel na Marekani katika kuleta usalama.
Amesema Nyanja muhimu ya msaada wa Marekani kwa Nigeria na nchi nyingine za ukanda wa Sahel ni kuimarisha uwezo wa majeshi ya usalama kwa njia ya vitendea kazi, tekinolojia na kupeana taarifa za kijasusi.