1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boakai atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Liberia

21 Novemba 2023

Mwanasiasa mkongwe Joseph Boakai ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Liberia, akimshinda rais aliyekuwa madarakani George Weah.

Liberia | Uchaguzi wa urais
Rais mteule wa Liberia Joseph Nyumah BoakaiPicha: Pulloh Moh-Marsi/Matrix Images/picture alliance

Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya uchaguzi NEC Davidetta Lansanah amewaambia waandishi wa habari kuwa Boakai ameshinda kwa asilimia 50.64 ya kura dhidi ya asilimia 49.36 ya kura alizopata nyota wa zamani wa soka George Weah.

Rais huyo mteule ameshinda kwa tofauti ya kura 20,567 pekee.

Weah alikuwa tayari amekubali kushindwa kufikia Ijumaa jioni kutokana na matokeo ya zaidi ya asilimia 99 ya vituo vya kupigia kura kuonyesha mpinzani wake alikuwa amemshinda kwa mbali.

George Weah ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora duniani ya Ballon d'or mwaka 1995, amepata sifa kimataifa kwa kukubali kushindwa na kukabidhi madaraka bila ya vurugu.

Rais wa Marekani Joe Biden ametuma pongezi kwa Boakai huku akimsifu George Weah kwa "kuheshimu chaguo la watu na kwa kuonyesha uzalendo."

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW