Boateng, Hummels kukosa mchuano dhidi ya Gibraltar
8 Juni 2015Matangazo
Ujerumani itashuka dimbani katika mchuano wa kirafiki dhidi ya Marekani mjini Cologne siku ya Jumatano kabla ya kupambana na Gibraltar katika mchuano wa kufuzu katika dimba la mataifa ya Ulaya - Euro 2016. Mpambano huo utachezwa mjini Faro, Ureno siku tatu baadaye.
Manuel Neuer, Thomas Mueller na Toni Kroos wameachwa nje ya kikosi lakini Patrick Herrmann wa Borussia Moenchengladbach amepewa fursa ya kucheza. Mats Hummels wa Borussia Dortmund alijiondoa jana katika timu ya taifa kutokana na maumivu ya nyonga lakini nafasi yake imejazwa na Jerome Boateng wa Bayern Munich.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu