BOGOTA: Waasi waachilia watalii wa kigeni
23 Desemba 2003Matangazo
Waasi wa Colombia wameaachilia huru watalii 5 wa kigeni waliokuwa wametekwa nyara miezi 2 iliopita. Watu hao ni Waisraili 4 na raia mmoja wa kingereza ambao walikuwa miongoni mwa wageni 8 waliokamatwa na waasi wa mrengo wa kushoto karibu na milima ya Sierra Nevada. 2 kati yao ambao ni Mjerumani na Muhispania waliaachiliwa huru mwezi uliopita. Mwengine wa nane ambaye ni Mwingereza alifaulu kutoroka muda mfupi baada ya kutekwa nyara na waasi hao wa Colombia.