BOGOTA:Maofisa 14 wa polisi nchini Colombia wauawa kwa bomu la kutegwa barabarani.
2 Agosti 2005Polisi wa Colombia wameeleza kuwa bomu liliolokuwa limetegwa barabarani,limesababisha vifo vya maofisa wake 14 katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.Tukio hilo limetokea wakati maofisa hao wa polisi walipokuwa ndani ya basi karibu na milima ya Sierra Nevada iliyopo katika jimbo la Cesar.Maofisa wa polisi wa Colombia wamekishutumu kikundi cha waasi wa Marxist-FARC kuhusika na shambulio hilo.
BOGOTA: Shambulio hilo limetokea wakati kukiwa na mpango wa amani wenye lengo la kuwapokonya silaha wanamgambo wa nchi hiyo.
Zaidi ya wanamgambo 2,000 wenye kufuata siasa za mrengo wa kulia walikabidhi silaha jana siku ya Jumatatu,katika sherehe zilizohudhuriwa na kiongozi wao Diego Murillo pamoja na msuluhishi kutoka upande wa serikali.Luis Carlos Restrepo.Serikali ya Marekani inamtuhumu Bwana Murillo kuwa ana jihusisha na biashara ya dawa za kulevya.