1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Bolsonaro apanga kurejea Brazil katika wiki zijazo

12 Februari 2023

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro amesema usiku wa jana Jumamosi kuwa anapanga kurejea Brazil katika wiki zijazo.

USA Miami | Jair Bolsonaro
Picha: Chandan Khanna/AFP/Getty Images

Bolsonaro aliwasili nchini Marekani Desemba mwaka jana, siku chache kabla ya wafuasi wake kuvamia majengo ya serikali huko Brasilia katika jaribio la kupinga ushindi wa mpinzani wake, Luiz Inacio Lula da Silva.

Bolsonaro, mwenye umri wa miaka 67, anakabilia na uchunguzi nchini Brazil ili kubaini jukumu lake katika shambulio la Januari 8 dhidi ya taasisi za kitaifa.

Bolsonaro amesema kufuatiliwa kwake si halali maana aliongoza bila ufisadi na kufanya kazi kwa moyo moja na kwa uaminifu.

Tukio la Brasilia  limekuwa likilinganishwa na shambulio la Januari 6, mwaka 2021 katika Bunge la Marekani lililoendeshwa na wafuasi wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW