1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolsonaro arejea Brazil kuongoza upinzani dhidi ya Lula

30 Machi 2023

Rais wa zamani wa Brazil wa siasa kali za mrengo wa kulia Jair Bosonaro, amerejea nyumbani kutoka uhamishoni jimboni Florida, Marekani kuuongoza upinzani dhidi ya rais wa siasa za mrengo wa kushoto Luiz Inacio da Silva.

USA, Florida | Brasiliens Ex-Präsident Jair Bolsonaro
Picha: Rebecca Blackwell/AP/picture alliance

Maelfu ya wafuasi wamemkaribisha kiongozi huyo ambaye hakukubali kushindwa katika uchaguzi wa mwaka jana, katika uwanja wa ndege wa Brasilia.

Maafisa waliimarisha usalama, kwa kufunga barabara za kuelekea katika maduka makubwa ya mji huo ili kuzuia hatari ya kuzuka maandamano yenye vurugu.

Bolsonaro apanga kurejea Brazil katika wiki zijazo

Bolsonaro alikimbilia Marekani, siku mbili kabla ya kukabidhi madaraka kwa Lula mnamo Januari mosi.

Alisema alihitaji kupumzika, lakini wakosoaji wanasema alikuwa anakwepa hatari ya kufanyiwa uchunguzi wa kisheria wa kesi kadhaa ambazo huenda akakabiliwa nazo nchini Brazil.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW