SiasaPeru
Boluarte:Bunge idhinisheni uchaguzi wa mapema
30 Januari 2023Matangazo
Kupitia hotuba aliyoitoa usiku wa kuamkia leo, kiongozi huyo amesemabunge linapaswa kuridhia uchaguzi mkuu ufanyike mwishoni mwa mwaka huu badala ya tarehe ya sasa ya April mwaka 2024.
Wabunge wa nchi hiyo wanakutana kwa mara nyingine leo kujadili pendekezo hilo la serikali baada ya kulikataa siku ya Jumamosi.
Soma pia:Wabunge wa Peru wawasilisha ombi la kumng'oa rais Boluarte
Rais Boluarte amesema iwapo wabunge watashindwa kutoa idhini ya kufanyika kwa uchaguzi mnamo mwezi Disemba atalazimika kupendekeza marekebisho ya katiba kushinikiza mpango huo.
Hadi sasa watu 48 wameuwawa tangu Peru ilipotumbukia kwenye mzozo wa kisiasa uliochochewa na kuondolewa madarakanimwaka jana kwa rais wa wakati huo Pedro Castillo.