1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bomu la nuklia la Korea ya kaskazini na athari zake:

26 Mei 2009

ndio mada kuu iliowashughulisha leo wahariri wa Ujerumani:

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani, leo yamechambua malalamiko ya wakulima wa Ujerumani na mada nyengine za ndani.Mada iliochambulłiwa kwa mapana zaidi lakini, ni jaribio la bomu la nuklia lililofanywa jana na Korea ya Kaskazini.

"Mtihani wa kwanza kwa rais barack Obama katika siasa za nje hautakawia kuja -alisema mpinzani wa Obama wakati wa kampeni ya uchaguzi akiashiria kutokomaa kisiasa kwa rais Obama.Korea ya kaskazini ndio sasa mtihani wenyewe."

Ama gazeti la Berliner Morgenpost laandika kwamba, Kiongozi mpenzi wa Korea ya Kaskazini anaufanyia dhihaka ulimwengu akiwa na azma mbaya.Labda kwanza hakusudii vita dhidi ya Korea ya Kusini,zaidi ni kuwatia shindo maadui zake na kuudumisha utawala wake kukabili shinikizo la aina yoyote kutoka nje pamoja hata na China.Kwa njia hii lakini Mapatano ya kutoeneza silaha za kinuklia yanavunjika.Kwani, kule Korea ya kaskazini inakoongoza, zitafuata nchi nyengine.Morgenpost likaongeza:

"Kile kilichoanzishwa sasa huko mashariki ya mbali,alitaka rais John F.Kennedy kukizuwia kwa kufungwa mkataba wa kukataza kuenezwa silaha za kinuklia.Je, silaha zote za kinuklia sasa zikomeshwe kuwapo ?

Kile dola kuu zenye nguvu na wale wenye nia njema wanachodai ,hakina nafasi kubwa ya mafanikio...."

Likiendeleza mada hii,gazeti la ABENDZEITUNG kutoka Munich,laandika kuwa licha ya kitisho cha vita vya kinuklia kilivyokuwa kikubwa zama za vita baridi,kilibakia ndani ya mashirika ya ulinzi ambayo leo hayapo .Leo kuna watu kama Kim ambao hawana kingine isipokuwa kutishia kwa mabomu ili kuseleleza utawala wao.

Gazeti laongeza:

"Hujuma itakayofanywa na Kiongozi huyo ikisabababisha vifo vya maalfu ya wanadamu, itaubadili ulimwengu........Rais Barack Obama ameelezea mawazo kuwa na dunia isio na silaha hizi za kinuklia, kwavile, alikwishatambua hatari hii.Kuanzia jana mawazo yake hayo, yamegeuka kuwa ndoto tu."

Likitubadilishia mada, gazeti la MUNCHNER MERKUR linazungumzia malalamiko ya wakulima wa Ujerumani na madai yao kuwa bei za maziwa yao ziko chini sana:Gazeti laandika:

"Wiki 2 kabla ya uchaguzi wa Bunge la ulaya na miezi 4 kabla ya uchaguzi mkuu wa Ujerumani,shinikizo la miezi kadhaa la wakulima ambao hali zao za maisha zimo hatarini,athari zake za kwanza zimechomoza:

Serikali ya Muungano ya Ujerumani mjini Berlin, imewaregezea kamba ,kwani alao kwa kipindi cha miaka 2 ijayo, wakulima hawatatozwa kodi kwa nishati ya diesel wanayotumia..... Ni vyema kuiona serikali ya Ujerumani inaonesha sasa vitendo katika kuwahurumia wakulima .Bei ya maziwa lakini, serikali haiwezi kuamua , inaweza kuwapunguzia tu mzigo wa kazi zao za ukulima mashambani.Hatua ya kwanza imechukuliwa."

Gazeti la NEUE WESTFALISCHE linaongea juu ya ujira mdogo wanaolipwa madereva wa mabasi.Laandika:

"Sio tu bei za maziwa hapa nchini ziko chini,bali pia ujira wa wafanyakazi ni mdogo na nchini Ujerumani, unanunuliwa kwa bei ya chini sana.Mishahara ya uonevu ipo leo takriban katika kila tawi la kiviwanda.Wakati basi umewadia kwa wafanyikazi kuonesha hawavumilii tena hali hiyo.Baadhi ya madereva wa mabasi wameshafanya hivyo.Wameshinda kwa kadiri fulani kesi yao mbele ya Mahkama ya mji wa Bielefeld..."

Mtayarishaji:Ramadhan Ali

Mhariri:Othman Miraji

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW