1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOMU LARIPUKA KABUL:

25 Desemba 2003

KABUL: Bomu limeripuka mapema leo hii katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul,nje ya nyumba inayotumiwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.Mripuko huo umeteketeza ukuta unaoizunguka nyumba hiyo.Madirisha mengi pia yamevunjika,lakini hakuna aliejeruhiwa.Bomu hilo limeripuka kiasi ya kilomita 8 kutoka Chuo Kikuu cha Kabul kunapofanywa mkutano wa kihistoria wa Baraza la Kikatiba.Hili ni shambulio la tatu kufanywa katika mji mkuu Kabul tangu kufunguliwa kwa mkutano wa Baraza hilo Desemba 4.Baraza hilo linakutana kujadiliana na kuidhinisha katiba mpya ya Afghanistan,ikitarajiwa kuwa mwakani nchini humo kutafanywa uchaguzi mkuu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW