1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bomu laua wafugaji 40 Nigeria

27 Januari 2023

Idadi ya watu waliokufa katika shambulizi la bomu dhidi ya kundi la wafugaji katikati ya Nigeria imefikia 40.

Nigeria Rigasa | Polizist am Bahnhof an der Abuja-Kaduna Zugstrecke
Picha: Olukayode Jaiyeola/NurPhoto/picture alliance

Gavana wa Jimbo la Nasarawa, Abdullahi Sule alisema jana kuwa idadi hiyo imeongezeka kutoka ya awali ya watu 27 waliouawa katika shambulizi lililotokea siku ya Jumatano huko Rukubi, kijiji kilichoko kwenye mpaka wa majimbo ya Nasarawa na Benue.

Sule amesema shambulizi hilo lilisababishwa na ndege isiyokuwa na rubani ambayo ilidondosha bomu, bila ya kutoa maelezo zaidi nani aliyekuwa akiiendesha ndege hiyo.

Soma zaidi: Wanamgambo 200 waliuwawa desemba katika mapigano Nigeria

Chama cha wafugaji, kimesema bomu hilo lilidondoshwa na ndege ya kijeshi ya Nigeria.

Wakulima na wafugaji katikati ya Nigeria wamekuwa wakizozana kuhusu haki za malisho na maji kwa miongo kadhaa, lakini ghasia zimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni baada ya baadhi ya wakulima kujiunga na magenge ya uhalifu ambayo yanavamia vijiji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW