BONN : Steimeier apongeza mchango wa Deutsche Welle
21 Septemba 2007Mkuu wa matangazo ya lugha za kigeni wa Radio Deutsche Welle Miodrag Soric amekuwa na mahojiano leo hii na Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir.
Mahojiano hayo yamehusu mada zitakazojadiliwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati litakapokutana wiki ijayo mjini New York Marekani.Mada hizo ni pamja na mzozo wa Iran,mageuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,juhudi za kupambana na kuzidi kwa hali ya ujoto duniani,mashariki ya kati na kadhalika.
Kuhusu mchango wa Deutsche Welle waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani Steinmeir amesema Deutsche Welle ni muhimu kwo kwa sababu inasikika katika pembe ambayo wao au wabunge na maafisa wengine wanakuwa wakiyatembelea.Na cha kusifiwa zaidi ni mchango wa Deutsche Welle katika kuimarisha mfumo wa vyama vingi,demokrasia na kupigania haki za binaadamu.
Steinmier anakwenda New York wiki ijayo kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.