1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKosovo

Borell alaani mauaji ya polisi huko Kosovo

24 Septemba 2023

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, amelaani shambulio la leo dhidi ya maafisa wa polisi nchini Kosovo lililosababisha kifo cha afisa mmoja na kujeruhiwa kwa maafisa wengine wawili.

Albanien Der Hohe Vertreter der EU für Außen- und Sicherheitspolitik, Josep Borell, auf der gemeinsamen Pressekonferenz in Tirana
Picha: Press Office, Albania Premiership

Katika taarifa yake, Borrell amesema kuwa ukweli wote kuhusu shambulio hilo unahitaji kubainishwa na aliyehusika kuwajibishwa.

Borrell ameongeza kuwa maisha zaidi ya watu wasio na hatia yamo hatarini katika mapigano yanayoendelea nchini humo hasa katika maeneo ya karibu na Banjska, na kutoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi hayo mara moja.

Borrell amesema pia kuwa Ujumbe unaosimamia utawala wa sheria wa Umoja wa Ulaya EULEX unawasiliana na mamlaka  nchini Kosovo pamoja na ujumbe wa kulinda amani wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, huku akirejelea wito wa Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama wa kusitisha uhasama katika eneo la Kaskazini mwa Kosovo, lenye idadi kubwa ya raia wa jamii ya Waserbia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW