1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boris Becker ana wasiwasi kuhusu ratiba ya tenisi

Josephat Charo
11 Mei 2020

Becker amesema anahofia ratiba ya mashindano ya tenisi mwaka huu huenda ikavurigika kabisa iwapo mashindano ya French Open na US Open yatafutwa kutokana na janga la COVID-19.

Tennis - Hamburg European Open - Boris Becker verfolgt Spiel
Picha: picture-alliance/dpa/D. Bockwoldt

"Nadhani mengi yatategemea uamuzi kuhusu mashindano ya US Open na French Open. Nafikiri litakuwa jambo la busara kwa pande zote husika kusubiri na kuangalia aina ya ugonjwa, athari zake zitadumu muda gani, lini maambukizi yatakapopungua badala ya kupitisha uamuzi wa haraka, alisema Becker.

"Kama mashindano ya French Open hayatafanyika, sidhani kama tutakuwa na mashindano ya tennis muda uliobakia mwaka huu." Aliongeza kusema.

Akizungumza na televisheni ya Reuters Jumanne (05.05.2020) Becker pia alisema kusimama kwa mchezo wa tenisi kwa muda mrefu kutawanufaisha nyota watatu Roger Federer, Novak Djokovic na Rafael Nadal, pamoja na Serena Williams na kumpa Andy Murray muda zaidi wa kupona kutokana na jera lake kwenye nyonga.

Akizungumza kuhusu hali ilivyo sasa Djokovic alisema binafsi anapinga chanjo na hangependa alazimishwe kudungwa chanjo ili aweze kusafiri.

Kwa upande wake Serena Williams amesema wakati wote mtu akipumua karibu naye au kukohoa anakereka na wakati mtoto wake msichana akikohoa anakasirika na kumuangalia kwa jicho la pembeni.

(rtrtv)