1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boris Johnson akabiliwa na shinikizo kuhusu janga la Corona

22 Aprili 2020

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametolewa mwito wa kuanzisha uchunguzi kuhusu jinsi serikali inavyolishughulikia suala la janga la virusi vya Corona

Coronavirus Premierminister Boris Johnson
Picha: Reuters/S. Dawson

Mwito huo umetolewa baada ya Waziri Mkuu Johnson kushindwa kutowa maelezo kamili kuhusu data za awali za waliokufa, kiwango kidogo cha waliopimwa au ukosefu wa vifaa vya hospitali.

Waziri mkuu huyo awali alijizuia kuidhinisha hatua kali za kudhibiti shughuli za kijamii ambazo viongozi wengine wa Ulaya walizichukuwa, lakini baadaye alitangaza kufunga kabisa shughuli zote zisizokuwa za lazima na watu kuzuiwa kutoka nje baada ya takwimu kuonesha robo ya watu milioni 1 huenda wakafa nchini Uingereza.

Hata hivyo tangu zichukuliwe hatua hizo serikali imekuwa ikitowa maelezo ya kutatanisha kuhusu kwa nini ilishindwa kuingia kwenye mpango wa Umoja wa Ulaya wa kupata mashine za kusaidia upumuaji, pamoja na kukiri kwamba yamekuwepo matatizo ya kupata vifaa vya kutosha vya kuwakinga wafanyakazi wa sekta ya afya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW