Borussia Dortmund yadhibiti kipindi cha kwanza cha ligi
24 Desemba 2018Borussia Dortmund huenda ina historia upande wake wakati wakiwa na uongozi wa pointi sita katika kipindi hiki cha mapumziko ya majira ya baridi lakini itakuwa ujinga kuwapuuzia Bayern Munich kwa kuwa ligi hii ya Ujerumani hatimaye itakuwa na mpambano mkali wa kuwania ubingwa kwa mara nyingine tena.
Dortmund imeweza kunyakua taji la ubingwa wakati wakiongoza katika kipindi hiki cha mapumziko ya katikati ya msimu , na vijana chipukizi wa kocha Lucien Favre wameng'ara katika michezo 17 iliyopita.
Ushindi mara 13, sare mbili na kipigo mara moja tu na tarakimu zilizo wazi wakati wakijikingia pointi 42, jumla ya pili bora katika historia ya klabu hiyo licha ya kuwa kocha mpya Lucien Favre ameomba kuwe na subri na kikosi chake kipya kuelekea mwishoni mwa msimu.
Usajili wa katikati ya mwaka
Lakini wachezaji walionunuliwa katikati ya msimu ambao ni pamoja na mlinzi Abdou Dialo pamoja na wachezaji wa kati Thomas Delaney na Axel Witsel hadi mshambuliaji Jadon sancho na Paco Alcacer wamekosha nyoyo wapenzi wa Dortmund pamoja na nahodha wao ambaye yuko katika kiwango cha juu Marco Reus wakati Dortmund ina matumani kwa mara ya kwanza kunyakua taji la ubingwa tangu mwaka 2012.
"Tunamatumaini tutaendelea kuwa fit na kuendelea kufanya vizuri. Kutokana na hali hiyo mengi yatawezekana," amesema Reus.
Dortmund inapata kujiamini sana katika kipindi hiki cha mapumziko wakati wakiumaliza mwaka kwa kurejea katika mafanikio baada ya kupata kipigo cha kwanza katikati ya wiki, dhidi ya timu iliyoko mkiani ya Fortuna Dusseldorf kwa kuishinda Borussia Moenchengladbach kwa mabao 2-1 katika kile kilichoelezwa kuwa ni pambano la timu zilizoko juu ya msimamo wa ligi siku ya Ijuma.
Mkurugenzi wa soka wa Gladbach Max Eberl ameitaja Dortmund kuwa wana uwezekano mkubwa wa kupata taji la ubingwa lakini ameonya kwamba "hakuna mtu anapaswa kuipuuzia Bayern.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae