1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia Dortmund yaibwaga Celtic 7-1

Josephat Charo
2 Oktoba 2024

Karimi Adeyemi alifunga mabao 3 katika kipindi cha kwanza katika ushindi wa 7-1 wa timu yake, Borussia Dortmund, dhidi ya Celtic katika pambano la ligi ya mabingwa Champions lililochezwa jana nyumbani Signal Iduna Park.

Borussia Dortmund yaibwaga Celtic 7-1
Borussia Dortmund yaibwaga Celtic 7-1Picha: Ralf Treese/DeFodi Images/picture alliance

Timu nyingine ya Ujerumani, Bayer Leverkusen, ilipata ushindi wa tabu wa bao 1-0 dhidi ya Milan nyumbani BayArena.

VfB Stuttgart walilazimishwa sare 1-1 nyumbani na Sparta Prag.

Soma zaidi: Dortmund yaanza kampeni ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Club Brugge

Katika matokeo mengine, Arsenal ilionesha ubabe Paris Saint Germain kwa kuicharaza mabao 2-0, huku Manchester City ikiitandika Slovan Bratislava goli 4-0.

Leo Bayern Munich inakwaana na Aston Villa huku RB Leipzig ikiwa na miadi na Juventus. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW