1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bosnia. Waserb walioendesha mauaji ya Waislamu huko Srebrenica wakamatwa.

25 Juni 2005

Waserb 11 kutoka Bosnia wamekamatwa kwa kuhusika na majuaji ya mwaka 1995 katika mji wa Srebrenica.

Ripoti za vyombo vya habari vya nchi hiyo zinasema kuwa watuhumiwa hao wote walikuwa ama maafisa wa zamani ama wale ambao bado wako kazini. Hatua hiyo ya kuwakamata imekuja kabla ya maadhimisho ya tukio baya kabisa katika bara la Ulaya la mauaji tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia.

Hapo Julai 11, 1995 kiasi cha wanaume 8,000 Waislamu pamoja na wavulana waliuwawa wakati majeshi ya Waserb wa Bosnia pamoja na vikosi vya polisi vya Serbia viliposhambulia eneo hilo lililokuwa likilindwa na majeshi ya kulinda amani ya umoja wa mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW