1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBosnia na Herzegovina

Bosnia yaadhimisha miaka 30 ya mauaji ya Srebrenica

8 Julai 2025

Zaidi ya watu 6,600 wameanza maandamano ya siku tatu ya kuaadhimisha miaka 30 tangu mauaji ya kimbari ya Srebrenica nchini Bosnia.

Makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Srebrenica huko Bosnia
Makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Srebrenica  huko BosniaPicha: Keno Verseck/DW

 Maandamano hayo yameanza leo mjini Sapna na yataelekea umbali wa kilomita 100 hadi katika kituo cha kumbukumbu ya  mauaji ya Srebrenica   huko Pontocari.

Wakati wa mauaji hayo yanayokumbukwa, mwaka 1995, zaidi ya wanaume na vijana 8,000 wa Kiislamu wa jamii ya Bosniak waliuawa  karibu na mji wa Srebrenica katika vita vya Bosnia.

Siku ya mwisho ya maandamano itaadhimishwa kwa hafla maalumu na siku inayofuata yatafanyika maziko ya waathiriwa wapya waliotambuliwa wa mauaji hayo ya halaiki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW