1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Ajali ya boti yaua takribani watu 50 Kongo Mashariki

3 Oktoba 2024

Takriban watu 50 wamefariki baada ya boti iliyokuwa imewabeba kupinduka katika Ziwa Kivu, mashariki mwa Kongo hii leo.Mashuhuda wameliambia shirika la habari la AP.

DR Kongo
Baadhi ya wakaazi wa Goma waliopoteza wapendwa wao katika ajali ya boti iliyozama Ziwa Kivu. Oktoba 03, 2024.Picha: Ruth Alonga

Idadi kamili ya waliokuwamo kwenye boti hiyo haikufahamika mara moja na kwamba ni watu watu wangapi waliokuwemo ndani ya boti hiyo na ni wangapi ambao wameangamia. 

Mashuhuda wamesema watoa huduma ya uokozi walisaidia kutoa miili 50 kwenye maji huku watu 10 wakinusurika na kupelekwa katika hospitali ya mtaa.

Ongezeko la maji Ziwa Tanganyika laathiri biashara Kigoma

03:15

This browser does not support the video element.

Maafisa wa Kongo mara nyingi wameonya dhidi ya upakiaji kupita kiasi na kuapa kuwaadhibu wanaokiuka hatua za usalama kwa usafiri wa majini.

Soma pia:Raia wakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula Goma

Lakini katika maeneo ya mbali ambako abiria wengi wanatoka, wengi hawawezi kumudu usafiri wa umma kutokana na uchache wa barabara.

Itakumbukwa pia mnamo  mwezi Juni, Boti iliyokuwa imejaa mizigo ilizama karibu na mji mkuu wa Kinshasa na abiria 80 walipoteza maisha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW