1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Botswana kuwa mthibitishaji almasi zinazokwenda G7

28 Novemba 2024

Kujumlishwa kwa Botswana kama mthibitishaji kunaonekana kukusudiwa kuokoa mpango wa utekelezaji wa marufuku dhidi ya almasi za Urusi, baada ya mataifa ya Afrika kulalamika kuwa uchumi wao utaathirika.

Botswana |  jiwe la almasi
Jiwe la almasi lililogunduliwa Botswana, la pili kwa ukubwa kuwa kuchimbwa wakati huo.Picha: Lucara Diamond Corp/picture alliance

Botswana, ambayo ni mmoja ya wazalishaji wakubwa wa almasi barani Afrika, itaungana na Antwerp kama mthibitishaji wa chimbuko la almasi ghafi kwa ajili ya kusafirishwa katika mataIfa ya G7, yaliopiga marufuku uagizaji wa madini ya Urusi kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

Ushirikishwaji wa Botswana unalenga kushughulikia wasiwasi wa wazalishaji wa Afrika kuhusu usawa wa kiuchumi. Mfumo wa awali wa uthibitishaji ungeshuhudia almasi zote zikipitia kitovu cha almasi cha Ulaya mjini Antwerp kwa ajili ya uhakiki, kwa kutumia teknolojia mpya ya ufuatiliaji.

Almasi ya pili kwa ukubwa duniani yapatikana Botswana

01:26

This browser does not support the video element.

Lakini wazalishaji wa almasi wa Afrika, mataifa ya Angola, Botswana na Namibia, pamoja na kampuni ya uchimbaji ya De Beers, walisema mfumo huo haukuwa wa haki na kwamba ungeathiri uchumi wao.

Mfumo wa ufatiliaji ulipanswa kuanza kufanya kazi kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, lakini Umoja wa Ulaya ulichelewesha utekelezaji wake hadi Machi 2025.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW