Botswana kuwa mthibitishaji katika marufuku ya almasi
28 Novemba 2024Matangazo
Hii ni baada ya kupata uungwaji mkono mkubwa wa kuingizwa kwenye kundi la nchi zilizo na jukumu la kuthibitisha uchimbaji wa Almasi ghafi na kuzisafirisha Almasi hizo kwenda kwenye mataifa ya G7 ambayo yalipiga marufuku uagizaji wa Almasi kutoka Urusi.
Kushirikiswa Botswana katika mfumo huo mpya wa ufuatiliaji kunalenga kushughulikia wasiwasi kuhusu usawa wa kiuchumi wa wazalishaji wa barani Afrika, zikiwemo nchi za Angola na Namibia.
Mfumo huo wa ufuatiliaji ulipaswa kuanza mwezi Septemba mwaka huu, lakini Umoja wa Ulaya umeahirisha utekelezwaji wake hadi Machi mwaka ujao wa 2025.