1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Botswana yamwapisha rais mpya aliyekishinda chama tawala

9 Novemba 2024

Rais mpya wa Botswana Duma Boko ameapishwa jana Ijumaa baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa wiki iliyopita uliokiondoa madarakani chama kilichoitawala nchi hiyo kwa karibu miaka 60.

Rais mpya wa Botswana Duma Boko
Rais mpya wa Botswana Duma Boko.Picha: Monirul Bhuiyan/AFP

Rais aliyeondoka madarakani Mokgweetsi Masisi alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Boko akiwa pamoja na viongozi wakuu wa mataifa kadhaa ya Afrika Zimbabwe na Zambia.

Boko, mwenye umri wa miaka 54 alikula kiapo mbele ya maelfu ya watu waliokusanya kwenye uwanja wa taifa mjini Gaborone, siku tisa tangu chama chake cha Umbrella for Democratic Change (UDC) kukiangusha chama tawala cha Botswana Democratic Party (BDP) kwenye sanduku la kura.

Akilihutubia taifa baada ya kula kiapo Boko amesema uchaguzi uliopita ulikuwa kipimo kwa demokrasia ya nchi hiyo na kwamba ushindi wake unafungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini Botswana.

Chama cha Boko cha UDC kilishinda viti 36 vya bunge ikilinganishwa na  4 pekee vya kilichokuwa chama tawala cha BDP, matokeo yaliyodhihirisha kukataliwa kwa chama hicho kilichoiongoza Botswana tangu uhuru mwaka 1966.