1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBrazil

Brazil: Miji yafuta kanivali kufuatia mafuriko

21 Februari 2023

Zaidi ya watu 36 wamefariki dunia kufuatia mvua kubwa ambayo imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Brazil.

Brasilien Unwetter l Zerstörung nach heftigem Regen in Sao Sebastiao
Picha: Sao Sebastiao City Hall /AFP

Miji miwili iliyoathiriwa zaidi na mvua hiyo kubwa  iliyonyesha pwani ya kusini mashariki mwa Brazil siku ya Jumapili, ni Sao Paulo na Bertioga.

Meya wa Sao Paulo  Tarcisio de Freitas amethibitisha hayo na kuongeza kuwa zaidi ya watu 800 wameachwa bila makaazi kufuatia mkasa huo.

Dde Freitas ametangaza hali ya tahadhari katika miji mitano ya pwani nchini humo.

Hapo jana, rais wa  Brazil Luiz Inacio Lula da Silva alizuru maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko ya Sao Paulo. Alitaka wanaoishi mabondeni eneo hilo kuhamishwa hadi maeneo salama

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW