1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRAZIL NI MABINGWA WA COPA AMERIKA.ENYIMBA NA ESPERENCE ZANGURUMA KAMA SIMBA KATIKA KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA NA MICHAEL SCHUMACHER ASHINDA HOCKENHEIM .

26 Julai 2004

MICHEZO

COPA AMERICA-Kombe la mataifa la Amerika Kusini:

Mabikngwa wa dunia Brazil wameongeza jana taji jengine walipoitimua Argentina kwa mabao 4-2 ya mikwaju ya penalty.hii inafuatia kutoka suluhu mabao 2:2 hadi firimbi ya mwisho na mikwaju ya penalty kubidi kuamua hatima ya Kombe hili.

Brazil ilisawazisha sekunde za mwisho wakati Argentina ikiongoza kwa mabao 2:1.Cesar Delgado aliipatia Argentina bao la pili mnamo dakika ya 87 ya mchezo.Adriano stadi chipukizi wa Brazil akaswazisha katika dakika ya 3 ya muda wa kufidia takriban katika mkwaju wa mwisho kabla firimbi kulia.

Brazil ilioitoa pia Uruguay katika nusu-finali kupitia changamoto ya mikwaju ya penalty, haikufanyxa mara hii pia makosa.Adriano,Edu,Diego na Juan-wote walitia mabao yao ya penalty na kuipatia Brazil chini ya kocha wake Carlos Alberto Parreira taji lao la 7 la Copa America.

Katika dimba la kirafiki huko Chicago,marekani, Bayern Munich iliitoa jana pia manchester United ya Uingereza kupitia mabao 4-2 ya mikwaju ya penalty.Alan Smith alikosa kuunasa wavu wa Bayern Munich.Umati wa mashabiki 58,121 ulisheheni uwanjani kuangalia mapambano huo uliovunja moyo ambao ulimalizika bila ya bao.bayern Munich imecheza mpambano 1 tu wakati manchester uinaendelea na mashindano haya ya Chicago .Mpambano wake ujao utakua dhidi ya Glasgow Celtic.Chelsea ilianza dimba hili kwa kuikomea Celtic mabao 4-2 huko Seatle.

VIKOMBE VYA KLABU BINGWA AFRIKA:

Changamoto za Kombe la klabu bingwa na Kombe la Shirimkisho zilikuwa uwanjani mwishoni mwa mwa wiki:

katika Kombe la klabu bingwa, mabingwa Enyimba kutoka Nigeria waliwashikisha adabu Bakili Bullets wa Malawi kwa kuwazaba mabao 6-0na hivyo imeparamia kileleni mwa kundi hilo.

Esperence ya Tunisia ikatamba nayo mbele ya Jeanne d’Arc ya Senegal kwa kuikumta mabao 5-0.USMA ya Algeria iliitoa SupedrSport ya Afrika Kusini kwa mabao 2:1 . Baada ya kumaliza mara mbili makamo-bingwa,Esperence imepania mara hii kulitwaa Kombe kwa mara nyengine tena tangu ilipolitwaa 1994.

Katika kombe la Shirikisho ,Petro Atletico ya Angola ilizusha msangao katika duru hii ya tatu ya kombe hili baada ya kutoka na ushindi wa bao 1:0 mbele ya FAR ya Rabat-klabu ya Jeshi.

Asante Kotoko ya Ghana imekamilisha maafa ya timu za Morocco mwishoni mwa wiki hii ilipotia bao la dakika ya mwisho la kusawazisha kufanya bao 1:1 na Waydad Casablanca ya Morocco.

Kotoko inasonga mbele kufuatia ushindi wa mabao 3:1 kutoka duru zote mbili.

Miongoni mwa klabu nyengine zinazosonga mbele katika kombe hili la shirikisho ni Al Hilal ya Sudan,Cotonsport Garoua ya kamerun,Enugu rangers ya Nigeria,Hearts of oak ya Ghana na Santos ya Afrika Kusini.

Nafasi ya mwisho kuingia duru ijayo pamoja na timu hizo,itaamuliwa kati ya mpambano baina ya Sable Batie ya kamerun na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Michezo ijayo ya Olimpik mjini Athens,Ugiriki itafunguliwa rasmi Augsut 13 na kuendelea hadi August 29.Miaka 4 iliopita, rais wa zamani wa Halmashauri kuu ya Olimpik (IOC) Juan Antonio Smaranch alionya waandazi wa michezo ya Athens hatari ya kupoteza nafasi ya kuiandaa michezo hii kwa kuchelewa-chelewa:

Sasa rais wa IOC ni Mbelegi Jacques Rogge na mji wa Athens, imetokwa na jasho hadi dakika ya mwisho kuwa tayari kwa ufunguzi hapo august 13.Na kwa mara ya kwanza tangu michezo ya Olimpik ya Moscow, 1980 ,rais mwengine mbali na Juan Antonio Samaranch ataitangaza michezo hii imefunguliwa rasmi-nae ni Jacques Rogge.

Miaka ya kati ya 1970ini wakati Uganda,ikijivunia bingwa wake wa olimpik wa Munich 1972, Tanzania ikivuma na Philbert Bayi-na kilele cha michezo ya Montreal,1976 kilikua kiwe changamoto katika mita 1500 kati ya John Walker wa NZ na Mtanzania Philbert Bayi.Changamoto hiyo haikutokea,kwavile tanzania kama nchi nyingi za kiafrikka ziliisusia michezo ya Olimpik ya Montreal.Miaka 4 baadae,

Bingwa wa dunia wa mbio za magari-mjerumani Michael Schumacher, jana aliwika tena kwa ushindi wake wa 11 kati ya 12 mwaka huu huko Hockenheim,nyumbani ujerumani.Nafasi ya pili alikuja Jenson Button wa Uingereza.

Kama katika mbio za baiskeli za Tour de France jana ambamo Muamerika Amstrong alinyakua ushi ndi wake wa 6 na kubainisha hashindiki, ku na wanaodai nao kwamba Michael Schumacher katika mbio za magari hakuna awezae kufua dafu mbele yake.

binafsi mwenyewe lakini anadai kwamba msimu huu atashindwa tena alao katika mbio moja nyengine.Michael Schumacher kama Amstrong.ni bingwa mara sita wa mbio za magari kama Amstrong wa mbio za baiskeli.

Mashindano yajayo baada haya ya jana huko Hockenheim,Ujerumani ni yale ya Budapest,Hungary mwezi ujao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW