Brazil yaahidi usalama wakati wa Olimpiki
11 Machi 2016Waziri wa UIinzi wa Brazil Aldo Rebelo anasema anatarajia kuwa maafisa wa usalama 85,000, wakiwemo wanajeshi 38,000 watatosha kuhakikisha usalama wakati wa mashindano hayo ya Rio de Janeiro kuanzia Agosti tano hadi 21. "kuhusiana na uwezekano wa ikiwa kutakuwa au hakutakuwa na maandamano ya umma, nadhani hayakutakuwapo. Sidhani kama tutashuhudia maandamano kama ya 2013 na kidogo mwanzoni mwa Kombe la Dunia 2014 kwa sababu wakati wa Kombe la Dunia 2014 hofu ilitulizwa sana. Nadhani Olimpiki itakuwa na mazingira tulivu zaidi ukilinganisha na 2013".
Baadhi ya makundi ya wakaazi wa Rio de Janeiro wameahidi kuandamana tena wakati wa michezo hiyo, hasa yale yanayowawakilisha watu walioachwa bila makaazi kutokana na miradi ya ujenzi kwa ajili ya Olimpiki.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Gakuba Daniel