1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoBrazil

Carlo Ancelotti kuinoa timu ya taifa ya Brazil kuanzia 2024

5 Julai 2023

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye shirikisho la soka nchini Brazil CBF kupitia Rais wake Ednaldo Rodriguez limetangaza kuwa Carlo Ancelotti atabeba mikoba ya timu ya taifa ya Brazil mwaka 2024.

UEFA Champions League Finale | Liverpool FC vs Real Madrid
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti atachukua mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya Brazil Selecao wakati wa mashindano ya Copa America mwakani 2024.Picha: Adam Davy/PA Wire/dpa/picture alliance

Shirikisho la soka nchini Brazil limetangaza kuwa kocha Carlo Ancelotti atakuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil kuanzia mwaka ujao.

Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) limesema leo kwamba meneja huyo wa Real Madrid atachukua mikoba ya timu ya taifa baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa na wababe hao wa Uhispania mnamo Juni 2024.

Soma zaidi: Vinícius Junior aishtumu La Liga kwa kutopambana na ubaguzi

Fernando Diniz, ambaye kwa sasa anaifundisha Fluminense, atakuwa kocha wa muda wa Brazil hadi Ancelotti atakaporejea kazini, CBF imethibitisha leo, Kocha atachukua nafasi hiyo wakati wa michuano ya Copa America ya 2024, itakayofanyika Marekani mwezi Juni na Julai.

Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil.Picha: Heuler Andrey/Action Plus/picture alliance

 Rais wa CBF Ednaldo Rodriguez amesema  ''Diniz ndiye kocha mpya wa timu ya taifa na kandarasi ya miezi 12 na tunafahamu kwamba kuna makocha wengi wazuri nchini Brazil, lakini amefanya kazi ya kiubunifu, kutoka kwa Audax, akiwa na falsafa nzuri, kila mara njia sawa na upya katika matumizi ya mbinu."

Soma zaidi:Ulaya na Brazil kukamilisha makubaliano ya biashara

Timu ya taifa ya Brazil ya Selecao imekuwa ikipambana kurejea katika ubora wake unaofahamika kote ulimwenguni hasa katika michuano ya kombe ya kombe la dunia na yale ya barani humo ya Copa America.

Ancelotti,mwenye umri wa miaka 64, amekuwa na kazi nzuri ya ukocha akiwa na vilabu vya AC Milan, Juventus, Chelsea na Real Madrid lakini kazi hii akiwa na Brazil itakuwa yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa.