Brazil yapokea uenyekiti wa G20
10 Septemba 2023Matangazo
Waziri mkuu wa India Narendra Modi amekamilisha kipindi chake na kukabidhi uenyekiti huo wa kupokezana kwa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva.
Baada ya kupokea kiti hicho, Lula amesema kuwa "masuala ya kijiografia ya kisiasa" hayapaswi kukwamisha majadiliano ya G20, akimaanisha malumbano ya kidiplomasia kuhusu vita vya Ukraine.
Viongozi wa G20 wamekuwa na mvutano mkubwa juu ya vita hivyo, tangu vilipoanza mwaka jana, huku Rais wa UrusiVladimir Putin akikosa kuhudhuria mkutano huo ili kukwepa mzozo wa kisiasa.