1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaBrazil

Brazil yarekodi vifo vya kwanza vilivyotokana na Oropouche

26 Julai 2024

Brazil imerekodi vifo vya kwanza duniani vilivyotokana na virusi vya Oropouche baada ya wanawake wawili kufariki kutokana na ugonjwa huo unaoambukiza wanadamu kupitia nzi na mbu.

Mhudumu wa afya akinyunyiza dawa ya kuua mbu aina ya Aedes aegypti kusaidia kupunguza mripuko wa homa ya dengue nchini Brazil.
Mhudumu wa afya akinyunyiza dawa ya kuua mbu aina ya Aedes aegypti kusaidia kupunguza mripuko wa homa ya dengue nchini Brazil.Picha: Ueslei Marcelino/REUTERS

Wizara ya afya nchini Brazil imesema wanawake hao kutoka jimbo la Bahia kaskazini mashariki mwa Brazil walikuwa chini ya umri wa miaka 30 na walionyesha dalili za homa kali ya dengue.

Wizara hiyo imeongeza kuwa, imeorodhesha wagonjwa 7,236 waliokutwa na virusi vya Oropouche mwaka huu pekee japo wengi wameripotiwa kutoka majimbo ya Amazonas na Rondonia.

Soma pia: Tanzania yakiri kuwa na Chikungunya, Dengue

Tovuti ya kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani imeeleza kuwa, kuna mripuko wa ugonjwa wa Oropouche nchini Bolivia, Brazil, Colombia, Cuba na Peru.

Dalili za mgonjwa wa Oropouche hufanana na homa ya dengue na hudumu kati ya siku tatu hadi sita. Dalili hizo ni pamoja na maumivu ya misuli, viungo, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutapika na mgonjwa kuhisi baridi mwilini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW