1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yatangaza msaada kwa familia zilizokumbwa na mafuriko

16 Mei 2024

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ametangaza kifurushi kipya cha msaada kwa mamia ya maelfu ya wananchi wa kusini mwa taifa hilo waliokumbwa na mafuriko.

Mkoa wa Rio Grande do Sul
Mafuriko yaliyoukumba mkoa wa Rio Grande do SulPicha: Andre Penner/AP Photo/picture alliance

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ametangaza kifurushi kipya cha msaada kwa mamia ya maelfu ya wananchi wa kusini mwa taifa hilo waliokumbwa na mafuriko.Shughuli za kawaida zasimama Brazil huku mvua ikiendelea kunyesha

Serikali imesema itatoa karibu dola 1,000 kwa kila familia ili kuzisaidia kujenga upya maisha yao. Inakadiriwa kuwa kaya 240,000 zimeathiriwa na mafuriko hayo.

Rais Lula da Silva amelitembelea eneo lililoathiriwa zaidi la Rio Grande do Sul kwa mara ya tatu tangu mafuriko yaanze karibu wiki mbili zilizopita, na kusababisha vifo vya watu 149huku wengine zaidi ya nusu milioni wakilazimika kuyahama makazi yao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW