1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yatangaza siku saba za kumuomboleza Papa Francis

Josephat Charo
22 Aprili 2025

Brazil imetangaza siku saba za maombolezo kufuatuia kifo cha kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Kifo cha Papa Francis kimesababisha huzuni na simanzi kote ulimwenguni hasa miongoni mwa waumini wa kanisa Katoliki
Kifo cha Papa Francis kimesababisha huzuni na simanzi kote ulimwenguni hasa miongoni mwa waumini wa kanisa KatolikiPicha: Brazil's Sanctuary of Christ the Redeemer/AFP

Brazil, nyumbani kwa idadi kubwa kabisa ya waumini wa kanisa Katoliki duniani kote, itaomboleza kifo cha kiongozi mkuu wa kanisa hilo Baba Mtakatifu Francis kwa siku saba.

Akitoa tangazo hilo siku yaJumatatu rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva alisema ulimwengu umepoteza sauti ya heshima na hisani.

Waumini walishiriki ibada kote Brazil kumuombea papa Francis aliyefariki dunia mapema Jumatatu katika makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican akiwa na umri wa miaka 88.

Kwa mujibu wa ripoti ya Vatican ya mwezi Machi Brazil, nchi ya wakazi milioni 182, ndiyo yenye idadi kubwa ya Wakatoliki duniani kote.

Takwimu zinaonesha kiasi watu bilioni 1.4 ni sehemu ya kanisa Katoliki duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW