1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil:Dilma Rousseff apokonywa uongozi

Jane Nyingi31 Agosti 2016

Baraza la Senete la Bunge la brazil limepiga kura ya kumwondoa madarakani rais Dilma Rouseff na hivyo kuhitimisha utawala wa miaka 13 wa chama cha mrengo wa kushoto cha workers Party.

Brasilien Dilma Rouseff
Picha: Getty Images/AFP/E. Sa

Upinzani ulihitaji kura 54 miongoni mwa 81 za maseneta ili kumtimua Rouseff. Hata hiyo ulipata zaidi ya kura ulizotazamia baada ya ushindi mkubwa wa kura 61 dhidi ya 20.

Kundolewa kwa Rouseff sasa kunazua maswali mengi yasiyoweza kupata majibu kwa urahisi. Michel Temer ambae ni makamu wake, atahudumu muhula uliosalia hadi mwaka 2018 wakati wa kufanyika uchaguzi mkuu.Hata hivyo wabrazil tayari hameonyesha kutoridhika na utawala wake.

Wafuasi wa Dilma Rousseff akiandamana kukashifu uongozi wa Michel TemerPicha: picture-alliance/Zuma Press/C. Faga

Mwezi Mei baada ya kuteuliwa rais wa muda kufuatia kusimamishwa kazi Rouseff na Senete,mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 75 aliwatagaza mawaziri wake ambao wote ni wazungu, swala lilokashifiwa vikali, katika taifa hilo lilo na zaidi ya asilimia 50 ya watu wasiokuwa wazungu.

Mawaziri wake watatu walilazimika kujizulu wiki kadhaa baada ya kuanza kazi ,kutokana na kuhusishwa na rushwa,ambayo pia anamuandama Tremer. Washirika wa Rouseff wamesema watawasilisha rufaa katika mahakama ya juu ya nchi hiyo kupiga uamuzi huo.Mapema kabla ya kufanyika kura hiyo usalama ulimarishwa karibu na majengo ya baraza hilo la senete huku hali hiyo ikichangia msongamano mkubwa wa magari.

Baraza la Senete la bunge la BrazilPicha: Imago/Agencia EFE

Rouseff kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha workers party anatuhumiwa kwa udanganyifu wa fedha za bajeti muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2014 ili kuficha hali mbaya ya kiuchumi inayokabili taifa hilo,tuhuma alizokanusha vikali. Wakati akimtetea katika baraza la senete wakili wake Jose Eduardo Cardozo alimwondoa lawamani mteja wake."Kama kuna mtu aliyesahihi na msafi katika mfumo wa kisiasa wa Brazil uliokithiri rushwa ,ni Dilma Rouseff. Yeye havumilii rushwa,hata kamwe. Hajahusika kwa vyoyote katika ulaji rushwa, au hata kutuhumiwa" alisema Cardozo

Wachanganuzi wengi wa kisiasa walikuwa tayari wametabiri kuondolewa madarakani Rouseff. Chama chake cha workers party ambacho kimeongoza kwa zaidi ya mwongo mmoja nchini Brazil kimewaondoa watu millioni 29 katika lindi la umaskini.

Mwandishi:Jane Nyingi/afpw/ap

Mhariri: Iddi Ssessanga

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi