Bremen. SPD yaibuka kidedea.
14 Mei 2007Jimbo dogo nchini Ujerumani la Bremen limechagua bunge jipya, ambapo vyama vilivyokuwa hapo kabla vikiunda serikali ya mseto ya jimbo hilo vimepata pigo.
Chama cha Social Democratic kimepata asilimia 36.8, lakini hatimaye kimepata viti vingi zaidi.
Chama cha Christian Democratic, ambacho katika kiwango cha shirikisho kinaongozwa na kansela Angela Merkel , kimepata asilimia 25.6.
Chama cha Greens kimepata wingi zaidi na kumaliza kikiwa na asilimia 16.4.
Chama cha Left , au cha mrengo wa shoto kimepata kiti chake cha kwanza katika bunge upande wa magharibi ya Ujerumani. Mwakilishi wa chama cha Green jimboni Bremen Bärbel Hörn uchaguzi huo ni ishara ya kile kitakachotokea katika uchaguzi ujao wa majimbo nchini Ujerumani.
Meya wa chama cha Social Democratic katika jimbo la Bremen Jens Böhrnsen amesema kuwa anapanga kukamilisha mazungumzo ya mwanzo ya kuunda serikali ya mseto na chama cha Christian Democratic pamoja na cha Greens katika muda wa wiki mbili zijazo.