1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRICS yakubali wanachama wapya sita

24 Agosti 2023

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza mapema Alhamis kwamba kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi la BRICS litawakubali wanachama wapya sita.

Südafrika Johannesburg | BRICS Gipfel | Luiz Inacio Lula da Silva, Xi Jinping, Cyril Ramaphosa, Narendra Modi, Sergei Lavrov
Picha: Sergei Bobylev/TASS/dpa/picture alliance

Wanachama hao wapya ni Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Iran, Ethiopia, Argentina na Misri.

Ramaphosa alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa kilele wa kundi hilo mjini Johannesburg.

"Tumekubaliana katika awamu ya kwanza ya upanuzi na nyingine zitafuata. Tumeamua kuwakaribisha Argentina, Misri, Ehtiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kuwa wanachama kamili wa BRICS. Uanachama wao utaanza rasmi Januari Mosi mwaka 2024," alisema Ramaphosa.

Miito ya kulipanua kundi hilo, ambalo kwa sasa linaundwa na Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, ilitawala miongoni mwa ajenda katika mkutano huo wa kilele wa siku tatu na kuibua mgawanyiko miongoni mwa wanachama juu ya kasi na vigezo vya kuwakubali wanachama wapya.

Mkutano huo unahudhuriwa na wakuu wengine 50 wa serikali na mataifa, na unahitimishwa hii leo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW