1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRIGHTON : Waziri Mkuu wa Msumbiji ataka biashara huru

27 Septemba 2005

Waziri Mkuu wa Msumbiji Luisa Diogo hapo jana ameyataka mataifa tajiri kuyafunguwa masoko yao kwa nchi zinazoendelea na kusema kwamba uregezaji wa masharti ya biashara ni muhimu katika kusaidia kupunguza umaskini.

Diogo alipongeza makubaliano yaliofikiwa mapema mwaka huu na Kundi la Mataifa Manane Tajiri lenye maendeleo ya viwanda duniani kufuta madeni ya nchi 18 maskini kabisa duniani na kutowa msaada wa dola bilioni 50 kwa Afrika.

Lakini katika hotuba kwa mkutano wa kila mwaka wa chama tawala nchini Uingereza cha Labour Mama Doigo ameonya kwamba Malengo ya Maendeleo ya Milinea hayatoweza kufikiwa bila ya kuchukuliwa hatua za haraka zilizoratibiwa kwa pamoja.

Malengo hayo ni pamoja na kupunguza umaskini kwa nusu ifikapo mwaka 2015.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW