1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bronislaw Komorowski atarajiwa kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa Poland.

5 Julai 2010

Seikali yatangaza mkakati wa kubana matumizi kwa bajeti ya mwaka 2011.

Bronislaw Komorowski (Kushoto) anatarajiwa kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa Poland baada ya kumshinda,Jaroslaw Komorowski(Kulia),ambaye tayari amekubali kushindwa katika uchaguzi huo.Picha: picture alliance/dpa

Licha ya matokeo rasmi ya uchaguzi wa Poland yakiwa bado hayajatangazwa,matokeo yasiyo rasmi yanaonyesha kuwa,Rais aliyeshika madaraka ya muda kuiongoza nchi hiyo,Bronislaw Komorowski, anatarajiwa kutangazwa mshindi.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa leo,lakini zaidi ya asilimia 95 ya kura zilizohesabiwa,zinaonyesha kuwa Komorowski anaongoza kwa asilimia 52.6 dhidi ya 47,za Jaroslaw Kaczynski.

Komorowski aliteuliwa kuiongoza nchi hiyo katika kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu,kufuatia kifo cha ghafla cha Rais Lech Kaczynski kilichosababishwa na ajali ya ndege,ameahidi kumaliza msuguano wa kisiasa baada ya uchaguzi huo,kwa kufanya kazi pamoja na Chama cha Conservative.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa Komorowski pia anakabiliwa na changamoto ya kuendeleza mafanikio ya kiuchumi ya nchi

hiyo,ambao umetajwa kushika kasi zaidi miongoni mwa nchi 27 za umoja wa ulaya,ambapo chama chake cha Civic Platform,ndicho kinachoongoza serikali ya nchi hiyo.

Pacha wa Rais aliyefariki katika ajali hiyo,Jaroslaw Kaczynski amekiri kushindwa uchaguzi huo,na kumpongeza Komorowski,katika uchaguzi uliosimamiwa na Umoja wa Ulaya,na kueleza kuwa chama chake kinajipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa katika kipindi cha mpukutiko,na uchaguzi wa wabunge mwakani.

Poland itakuwa Rais wa Umoja wa Ulaya mwakani,kutokana na mfumo wa kupokezana nafasi za kuiongoza jumuiya hiyo.

Hata hivyo ushindi wa Komorowski katika kipindi cha miaka 5 ijayo,unaelezwa kuwa utapokelewa kwa furaha na Makao makuu ya umoja huo, pamoja na urusi,kutokana na msimamo wa chama cha Tusks kuhakikisha kunakuwepo maingiliano na nchi za nje,tofauti na kipindi kifupi cha Uwaziri Mkuu wa Jaroslaw Kaczynski mwaka 2006 -2007.

Pamoja na hayo,serikali ya nchi hiyo kupitia Waziri wa fedha,Jacek Rostowski ameeleza wazi kuwa bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka 2011 itazingatia zaidi kubana matumizi,na kuwataka wananchi,wanasiasa na bunge la nchi hiyo

kuiunga mkono,kwa kuwa na nidhamu nzuri ya fedha za serikali ili kuuinua uchumi wa nchi hiyo.

Katika utaratibu wa uendeshaji wa serikali nchini Poland,serikali inaandaa sera na kumpa mamlaka Rais kupendekeza na kuzipigia kura ya turufu,ambapo Hayati Lech Kaczynski alipiga kura yake ya turufu kwa miswada kadhaa kabla ya kifo chake,na kuwateua watendaji muhimu katika masuala ya nje na ya kiusalama.

Kutokana na hali hiyo,wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa Rais mtarajiwa Komorowski anapaswa kuyatumia mamlaka hayo kufanya mabadiliko makubwa aliyowaahidi wananchi wa Poland kabla ya kuchaguliwa kwake.

Kinyume na hayo,imeelezwa wazi kuwa chama cha Tusks kinaweza kushindwa katika uchaguzi wa wabunge mapema mwakani.

Mwandishi; Ramadhan Tuwa/ RTRE/AFPE

Mhariri;Mwadzaya,Thelma