1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa EU wapendekeza vikwazo dhidi ya Tanzania

27 Novemba 2025

Wabunge wa bunge la Umoja wa Ulaya wamependekeza kuweke vikwazo dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na matukio yaliyoambatana na uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29 nchini humo.

Straßbourg, Bunge la Ulaya
Bunge la UlayaPicha: Yves Herman/REUTERS

Wakati wa kikao cha bunge hilo kilichojadili hali ya kisiasa baada ya uchaguzi, wabunge hao wameutaka Umoja wa Ulaya kusitisha ufadhili wa kifedha kwa Tanzania. Wamesema ni lazima ufadhili huo uendane na maendeleo kwa kuzingatia utawala wa sheria, uwajibikaji na kulinda uhuru wa watu.

Matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji yatajwa

Wabunge wa bunge la Ulaya wamelaani pia nguvu kubwa dhidi ya waandamanaji, ukamatwaji wa kiholela na kufungwa kwa huduma za intaneti kwa siku kadhaa jambo lililozuia watu kupata taarifa.

Wamesisitiza kuwa Tanzania inahitaji uchaguzi huru na wa haki na pia wametoa wito wa kuachiliwa bila masharti kwa wafungwa wa kisiasa akiwemo Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, Tundu Lissu. Wametaka pia kuanzishwa kwa uchunguzi huru dhidi ya mauaji na matukio ya utekaji nyara.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW