BRUSSELS : ACP na Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano
26 Februari 2005Matangazo
Baada ya mazungumzo ya zaidi ya mwaka mmoja jana Umoja wa Ulaya na mataifa 77 yanoyojulikana kama ya ACP ya Afrika, Carribean na Pasifiki yamefikia makubaliano.
Miongoni mwa vipengele vya makubaliano hayo ni pamoja na serikali za mataifa ya ACP kujifunga kuchukuwa hatua madhubuti za kuzuwiya kuenea kwa silaha za maangamizi makubwa Kwa upande wake Umoja wa Ulaya umetangaza uko tayari kimsingi kuongeza msaada wa maendeleo lakini bila ya kuweka kima maalum.Umoja wa Ulaya bado haukuamuwa utaratibu wa kugawanya gharama za misaada hiyo miongoni wa mataifa yake wanachama.
Tafsiri mpya ya makubaliano ya Cotonou ya mwaka 2003 inatazamiwa kutiwa saini huko Luxembourg hapo mwezi wa Juni.