1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS. Bulgaria na Romania kujiunga na Umoja wa Ulaya.

14 Aprili 2005

Bunge la Umoja wa nchi za Ulaya limeyakubali maombi ya Bulgaria na Romania ya kutaka kujiunga na Umoja wa ulaya katika mkutano uliofanyika mjini Strasbourg.

Kukubalika kwa maombi ya nchi hizo mbili, sasa zitawajibika kutia saini mkataba katika dhifa maalum itakayofanyika huko Luxembourg Aprili 25.

Baadae mkataba huo utaidhinishwa na mabunge 25 ya mataifa yote wanachama wa umoja wa Ulaya.

Bulgaria na Romania zinatazamiwa kujiunga rasmi na Umoja wa nchi za Ulaya mwaka 2007 kwa masharti kuwa zitatimiza mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi ambapo ikiwa nchi hizi hazitatimiza masharti hayo basi huenda uwana chama wao ukacheleweshwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW