BRUSSELS: Cyprus na Malta kuanza kutumia Euro
16 Mei 2007Matangazo
Cyprus na Malta zimepata idhini ya Kamisheni ya Umoja wa Ulaya kutumia sarafu ya Euro kuanzia tarehe mosi Januari mwaka 2008.Uamuzi uliopitishwa leo hii umeondosha kikwazo kikubwa kabisa kwa nchi hizo mbili kujiunga na eneo linalotumia Euro.Kabla ya kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya,madola yanayoomba uanachama huo yanapaswa kutimiza malengo makali ya kiuchumi katika sekta za pesa,mfumko wa bei pamoja na viwango vya riba na ubadilishaji wa pesa.Kuanzia Januari ijayo,sarafu ya Euro itatumiwa katika nchi 15 kutoka jumla ya wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya.Jumla ya watu milioni 318 wanaishi katika eneo linalotumia Euro.