1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. EU kungalia njia za kupambana na ughali wa mafuta.

10 Septemba 2005

Mawaziri wa fedha wa umoja wa Ulaya wamo katika siku yao ya pili ya mazungumzo juu ya kupambana na ongezeko kubwa la bei ya mafuta pamoja na athari zake katika ukuaji wa kiwango cha chini wa uchumi wa mataifa hayo.

Mawaziri hao wa mataifa yanayotumia sarafu ya Euro wamekubaliana jana Ijumaa kuwa kupunguza kodi ya mafuta sio njia sahihi ya kupambana na hatari ya kudumaa kwa uchumi inayoletwa na bei kubwa ya mafuta.

Lakini waziri wa fedha wa Ufaransa Thierry Breton ameyalazimisha makampuni makubwa ya mafuta ya Total na BP kupunguza bei ya mafuta katika vituo vya kuuzia mafuta kwa kuyatishia kuyawekea kodi maalum katika mapato yao ya ziada .

Umoja wa Ulaya pia unaitaka Marekani kupunguza matumizi makubwa ya mafuta.

Wakati huo huo katibu mkuu wa shirika la mataifa yanayosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC , Adnan Shihab-Eldin amesema kuwa bei ya sasa ya mafuta ni kubwa mno na itabidi kushuka.

Ameyasema hayo katika mahojiano na jarida moja la Ujerumani , mahojaino ambayo yatachapishwa siku ya Jumatatu.

Shihab Eldin amesema kuwa mzozo wa kinishati umekwisha epukwa licha ya athari zilizoletwa na kimbunga Katrina , kimbunga amabcho kimeathiri uzalishaji wa mafuta katika ghuba ya Mexico , na kutabiri kuwa bei zitashuka.

Ameongeza kusema kuwa shirika lake halihitaji bei kubwa kama hizo za mafuta.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW