1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Mabadiliko ya sheria za jumuiya ya Ulaya ya bajeti yaidhinishwa na wakuu wa mataifa hayo.

23 Machi 2005

Viongozi wa jumuiya ya Ulaya wameidhinisha mabadiliko ya sheria za jumuiya hiyo za bajeti zinazoruhusu mataifa wanachama kuongeza matumizi yao. Mageuzi hayo katika maafikiano ya uthabiti na ukuaji ya jumuiya ya Ulaya , yanapelekea kuwa rahisi kwa nchi wanachama kama Ujerumani na Ufaransa kukiuka kiwango cha mwisho cha asilimia 3 cha nakisi ya bajeti, bila ya kuhofia kuwekewa vikwazo.

Katika mkutano wao wa siku mbili mjini Brussels, viongozi hao pia wanajadili pendekezo la tume ya jumuiya hiyo la kulegeza masharti ya masoko ya ndani. Hata hivyo baadhi ya mataifa yanapinga agizo hilo, wakisema kuwa litayaruhusu makampuni kutoka katika nchi moja mwanachama kuweka duka katika nchi nyimngine bila ya kuhitaji kufuata kanuni imara za kijamii.