1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Marekani na umoja wa Ulaya zaungana kuisaidia Irak

22 Juni 2005

Marekani na umoja wa Ulaya zimekubaliana kuisadia serikali ya Irak katika juhudi zake za kuijenga upya nchi hiyo. Serikali ya Baghdad imetakiwa kuhakikisha inawasaidia waislamu wa madhehbu ya suni nchini humo kuweza kujiendeleza.

Waziri mkuu wa Irak, Ibrahim al-Jafaari, alitoa wito kwa mataifa yanayohudhuria kikao hicho mjini Brussels kusadia kupambana na wimbi la machafuko la wapiganaji na kudumisha usalama nchini humo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleezza Rice amesema serikali mpya ya Irak ni lazima iongeze bidii katika kuboresha usalama, kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kuwafungulia milango ya kisiasa wairaki wote wanaoyapinga machafuko. Condoleezza Rice ameitaka Syria kuwazuia wanamgambo wanaolitumia taifa hilo kuweza kuingia Irak.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, amesema harakati muhimu za kisiasa zinaendelea, bila ya kujali kuungwa mkono au kupingwa kwa vita dhidi ya Irak.

Wakati huo huo, kundi la al-Qaeda nchini Irak limesema Marekani inautumia mkutano wa Brussels kuzuia kushindwa nchini Irak. Kundi la Abu Musab al-Zarqawi limesema maadui wa Mungu wanakutana Brussels kuiangamiza Irak, na wala sio kuijenga.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW