1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Matumizi ya Umoja wa Ulaya yazusha mgogoro

19 Juni 2005

Waziri mkuu wa Luxembourg,Jean-Claude Juncker ambae hivi sasa pia ni rais wa Umoja wa Ulaya amesema bara la Ulaya linakabiliwa na mgogoro mkubwa.Amesema hayo baada ya viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya kushindwa kuafikiana katika mkutano wao mjini Brussels juu ya bajeti ya hadi mwaka 2013 ya Umoja huo.Majadiliano yalivunjika baada ya viongozi hao kushindwa kuafikiana juu ya matumizi ya siku zijazo ikiwa ni pamoja na ruzuku zinazotolewa kwa Uingereza na misaada ya fedha kwa wakulima.Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amesema misimamo migumu ya Uingereza na Uholanzi ndio iliyosababisha kile alichokiita mgogoro wenye „hatari kubwa kabisa“ katika Umoja wa Ulaya.Viongozi wa nchi za Umoja huo vile vile hawakupitisha uamuzi kuhusu hatima ya katiba mpya ya Ulaya iliyopendekezwa.Lakini waliamua kuahirisha juhudi za kuidhinisha katiba hiyo,baada ya wapiga kura nchini Ufaransa na Uholanzi kuikataa katiba mpya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW