Brussels: Mawaziri wa fedha wa Umoja wa ulaya wamezuwia utaratibu...
26 Novemba 2003Matangazo
wa kuchukuliwa hatua Ujerumani na Ufaransa kwa kupindukia kiwango cha nakisi ya bajeti za nchi yao kama inavyotajwa ndani ya mkataba wa kudhamini utulivu wa sarafu ya pamoja-Euro.Uamuzi huo wa mawaziri wa fedha unakwenda kinyume na madai ya kamisheni kuu ya umoja wa Ulaya.Uamuzi huo unaokosolewa vikali na Hispania na mataifa mengine madogo madogo ya umoja wa ulaya umepelekea kuitishwa mkutano wa dharura wa benki kuu ya Umoja wa ulaya.Kuzuwiliwa utaratibu wa kuchukuliwa hatua nchi zinazopindukia viwango vya riba,kunaiwekea suala la kuuliza hatima ya mkataba wa kudhamini utulivu wa sarafu ya pamoja Euro.Benki kuu ya Ulaya imesema uamuzi wa mawaziri wa fedha umeitia dowa sera ya fedha ya umoja wa Ulaya.